PATA HABARI KWA WAKATI

Monday 4 November 2019

ZAERA AFUNGUKA MECHI YA NDANDA

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hakuwa na taarifa kuwa timu yake inapaswa kuelekea mkoani Mtwara ambako siku ya Ijumaa inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda Fc

Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili kutoka Misri leo, Zahera amesema hata viongozi wa Yanga hawakuwa wakifahamu

Hata hivyo amesema watajiandaa kikamilifu ili kuhakikisha wanapata ushindi kwani wanafahamu wanapaswa kufanya vizuri kwenye ligi ili wapate nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao

"Sikuwa nafahamu kama tunapaswa kwenda kucheza Mtwara baada ya mchezo dhidi ya Pyramids Fc. Hata viongozi hawakuwa wakifahamu, tumepata taarifa hiyo baada ya kurejea leo," amesema

"Tayari nimewataarifu wachezaji kuwa tunapaswa kuanza mazoezi kesho kujiandaa na mchezo huo"

"Baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Kimataifa, kipaumbele chetu ni kufanya vizuri kwenye ligi ili tupate nafasi ya kushiriki michuano hiyo msimu ujao"

Zahera amesema watakuwa na siku mbili za kufanya mazoezi kabla ya kuelekea mkoani Mtwara siku ya Alhamisi

No comments:

Post a Comment