PATA HABARI KWA WAKATI

Saturday 2 November 2019

Yanga imejichimbia hapa

Kikosi cha Yanga kiliwasili nchini Misri jana Alfajiri tayari kwa mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc
Mchezo huo utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa June 30 jijini Cairo
Katika kuhakikisha timu haikabiliwi na hujuma za aina yoyote, Yanga imefikia Hoteli ya nyota tano, The Guard ambayo inamilikiwa na Jeshi
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema mazingira ya hoteli hiyo ni salama, timu itafanya maandalizi yake bila ya bugudha
Aidha hoteli hiyo iko karibu na uwanja wa June 30 ambao utatumika kwenye mchezo wa kesho
Lakini pia haitakuwa na changamoto ya usafiri baada ya mchezo kwani hoteli hiyo iko karibu na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo

No comments:

Post a Comment