PATA HABARI KWA WAKATI

Tuesday 5 November 2019

MKWASA AMRITHI ZAERA YANGA

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kumteua Charles Boniface Mkwasa 'Master' kuwa kocha wa muda Yanga
Uamuzi huo umefikiwa baada ya Kamati ya Utendaji kuvunja benchi lote la ufundi la timu hiyo
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema Mkwasa ataiongoza Yanga katika kipindi cha mpito ambacho timu itakuwa ikisaka Mwalimu mwingine
"Timu imerejea mazoezini leo, kesho tunaelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda Fc ambao utapigwa Ijumaa"
"Wakati huu timu itakuwa chini ya kocha Charles Mkwasa 'Master' wakati tukikamilisha mchakato wa kumpata kocha Mwingine"
Inaelezwa tayari uongozi wa Yanga umemalizana na kocha wa Bandari Fc Ben Mwalala ambaye baada ya wiki mbili atajiunga na mabingwa hao wa kihistoria

No comments:

Post a Comment