PATA HABARI KWA WAKATI

Saturday 2 November 2019

MACHESTER UNITED MZIGONI LEO


MANCHESTER United leo ina kibarua kizito mbele ya Bournemouth mchezo wake wa ligi ikiwa ugenini. 

Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskajer amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo chanya. 

"Kila mchezaji kwa sasa ana morali kubwa ya kupambana kwa ajili ya timu ninatambua utakuwa mchezo mgumu ila tunachohitaji ni ushindi," amesema. 

United ipo nafasi ya 7 kwenye msimamo ikiwa imecheza jumla ya mechi 10 sawa na wapinzani wao Bournemouth ambayo ipo nafasi ya 9 na ina pointi 13.

No comments:

Post a Comment