PATA HABARI KWA WAKATI

Saturday 2 November 2019

KOCHA WA YANGA APATA SHAVU

Kocha wa zamani wa Yanga George Lwandamina ambaye kwa sasa anainoa Zesco United, ameteuliwa kuwa mshauri wa masuala ya ufundi timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo'

Lwandamina aliitumia Yanga msimu wa 2016/17 na 2017/18 akitokea klabu ya Zesco United kabla ya kuondoka kurejea klabu hiyo baada ya changamoto za kiuchumi kuikabili Yanga

Msimu huu timu yake ilikutana na Yanga kwenye raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa na kufanikiwa kutinga makundi kwa ushindi wa mabao 3-2

Ni mmoja wa makocha waliojijengea heshima kubwa nchini Zambia

No comments:

Post a Comment