PATA HABARI KWA WAKATI

Wednesday 4 December 2019

Kessy kurudi jangwani

Mlinzi wa Nkana Fc Hassan Ramadhani Kessy anahusishwa kurejea Yanga dirisha dogo la usajili ambalo litafunguliwa Disemba 16 2019

Kessy aliyeitumikia Yanga kwa misimu miwili kabla ya kuondoka msimu wa 2018/19, anaweza kurejea nchini kuungana na timu yake hiyo ya zamani

Wakati huu Yanga ina mapungufu kwenye safu ya ulinzi wa kulia, ikimtegemea Juma Abdul pekee baada ya Paulo Godfrey 'Boxer' kupata majeraha ambayo tayari yamemuweka nje kwa miezi mitatu mpaka sasa

Kabla ya kutimkia Zambia, Kessy alikuwa tayari kuongeza mkataba Yanga lakini hakuwa tayari kulipwa fedha za usajili kwa awamu

Wakati huo Yanga haikuwa vizuri kiuchumi hivyo kulazimika kumruhusu aondoke

No comments:

Post a Comment