PATA HABARI KWA WAKATI

Saturday 2 November 2019

VIWANJA VYA MTESA KOCHA SIMBA



PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba raia wa Ubelgij amesema kuwa tatizo kubwa linalowafanya wachezaji wake washindwe kucheza soka la darasani ni ubovu wa baadhi ya viwanja wanavyotumia.

Mbelgiji huyo amesema kuwa ni ngumu kwa ligi ya Bongo kuendelea iwapo tatizo la viwanja litafumbiwa macho kwani mchezaji bora anatengenezwa kwenye mazingira makini.

Akizungumza na Saleh Jembe, Aussems amesema kuwa lengo kubwa la timu yake ni kuona inashinda mechi zake zote licha ya ugumu wa viwanja vilivyopo.

“Maendeleo ya mpira yanahitaji uwekezaji na kupata matokeo wakati mwingine kunategemea na uwanja ambao wachezaji wanacheza ila kwa hapa kuna tatizo kwenye viwanja vingi kutokuwa kwenye ubora jambo ambalo linaua utamu wa soka.

“Haijalishi tunacheza uwanja gani kikubwa ambacho tunakitazama ni matokeo chanya, ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo tutapambana kupata atokeo chanya kwenye mechi zetu,” amesema Aussems.

Miongoni mwa viwanja ambavyo Simba imevitumia msimu huu ni pamoja na kile cha Karume, Mara dhidi ya Biashara United, Sheikh Amri Abeid dhidi ya Singida United, Kambarage dhidi ya Mwadui ambavyo Mbelgij alidai kuwa ubora wa uwanja ulikuwa hafifu.


No comments:

Post a Comment