PATA HABARI KWA WAKATI

Sunday 10 November 2019

OMOG KUTUA JANGWANI

Uongozi wa Yanga unaendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya baada ya kuvunja benchi lote la ufundi wiki iliyopita

Maombi yameendelea kumiminika ambapo miongoni mwa makocha waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Joseph Omog, kocha wa zamani wa Simba na Azam Fc

Omog aliipa Azam Fc ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2013/14, msimu ambao Azam iliibuka mabingwa bila ya kupoteza mchezo

Aliifundisha Simba kwa msimu mmoja ambapo Disemba 2017 alitimuliwa baada ya kuondoshwa kombe la Azam (ASFC) hatua ya awali na Green Worriors

Kocha huyo anayependelea soka la kushambulia, ameingia katika orodha ndefu ya makocha ambao wanawania kurithi mikoba ya Mwinyi Zahera aliyetimuliwa wiki iliyopita

Ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika. Pia amewahi kuzinoa klabu za AC Leopards (Congo) pamoja na timu ya Taifa ya Cameroon

Ben Mwalala, Hans van Pluijm, Kim Paulsen na Masudi Djuma ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kuwania nafasi hiyo

No comments:

Post a Comment