PATA HABARI KWA WAKATI

Thursday 21 November 2019

Beki kisiki wa Yanga Lamine Moro Mambo ni moto

Beki kisiki wa Yanga Lamine Moro amepona majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki kadhaa na yuko tayari kuitumikia timu hiyo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania hapo kesho

Moro aliumia katika mchezo wa mtoano kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc uliopigwa nchini Misri mapema mwezi huu

Moro pamoja na Ally Ally wote walishindwa kumaliza mchezo huo ambayo Yanga ililazimika kucheza na wachezaji 10 baada ya kuwa imemaliza 'sub' zote

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema mabeki hao wote wamepona

Bumbuli pia amebainisha kiungo Mohammed Issa 'Banka' amepona

Kama ikimpendeza Charles Mkwasa, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, anaweza kumtumia kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania hapo kesho

No comments:

Post a Comment