PATA HABARI KWA WAKATI

Tuesday 15 May 2018

Mechi ni kama mazoezi kwetu – Kocha wa Rayon Sport



Kocha mkuu wa timu ya Rayon Sports Ivan Minnaert, amesema kwamba timu yake imekua ikikosa muda wa kutosha wa kufanya mazoezi na hivyo timu hiyo kushindwa kujiandaa vya kutosha na michezo ya mashindano.

Kocha huyo amesema hayo leo Mei 15, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari kuelekea mechi ya mashindano ya kombe la Shilikisho barani afrika dhidi ya Yanga siku ya kesho na kuongeza kuwa timu yake inapumzika kwa siku mbili tu.

“Tumejaribu kadiri ya uwezo wetu hatukua na muda wa kutosha wa kujiandaa na mchezo, katika kipindi cha miezi miwili na nusu tumekua na siku mbili pekee za kufanya mazoezi, hivyo tunacheza mechi kila baada ya siku tatu kwahiyo unapopata siku mbili za kupumzika huwezi kuwa na muda wa kujiandaa na mchezo, kwahiyo kila mchezo ni kama mazoezi kwetu”, amesema kocha Minnart.

Awali mchezaji na nahodha wa timu ya Yanga Nadir Haroub “Cannavaro” amesema kuwa wamejiandaa vya kutosha ingawa wanaiheshimu timu ya Rayon Sports na kuwataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi.

“Tumejiaaandaa vizuri na mchezo wa kesho ila mchezo utakuwa mgumu, kwasababu Rayon (Sports) ni timu nzuri tunawaheshimu kwasababu ni mabingwa wa Rwanda, ila kwa upande wetu tumejiandaa vizuri na wachezaji ambao walipata majeraha wamerudi kama watatu nadhani ,kikosi kitaimalika kwa ajili ya mchezo wa kesho” aliongeza Cannavaro

Kesho Mei 16, 2018 timu ya Yanga itacheza mchezo wake wa pili wa kundi D dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda katika mashindano ya kombe la shirikisho la vilabu Barani Afrika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment