PATA HABARI KWA WAKATI

Monday 14 May 2018

Gor Mahia yatoka sare na Hull City uwanjani Kasarani, yapoteza kwenye matuta ya penalti



-Gor Mahia ilitoka sare tasa na Hull City kwenye muda wa kawaida

-Hata hivyo klabu hiyo ilipoteza mechi hiyo kwa ‘The Tigers’ kupitia matuta ya penalti

-Mechi hiyo ilikuwa ya kihistoria kwani klabu hizo zilikutana ugani kwa mara ya kwanza

Mabingwa wa ligi ya kitaifa (KPL) Gor Mahia ilitoka sare ya kutofungana bao lolote na klabu ya Hull City kwenye muda wa kawaida katika uwanja wa Kasarani Jumapili, Mei 23 kwenye mechi ya kirafiki.

Gor Mahia ilikutana na klabu hiyo ya ligi ya Uingereza baada ya kuishinda AFC Leopards uwanjani Afraha.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Pambano hilo lilikuwa la kihistoria kwa vilabu hivyo viwili huku Hull City ikizuru Kenya kwa mara ya kwanza kabisa.

Gor ilikuwa na washambulizi watatu, Blackberry, Guikan na Jacques Tuyisenge. Francis Kahata, Ernest Wendo na Humphrey Mieno wakiwa kwenye safu ya kati.

K’Ogalo walitajaria kuwa na fomu nzuri walioonyesha kwenye ligi ya humu nchini, lakini wakashindwa kwa mabao 4-3 kupitia mikwaju ya penalti.

Kipa Boniface Oluoch alizuia mikwaju miwili huku Harun Shakava na Onguso wakikosa kufunga mikwaju yao ya penalti.

Kabla ya pambano hilo, kocha wa Gor Mahia Dylan Kerr aliionya Hull City, akiahidi kuonyesha mchezo mzuri kwenye mechi hiyo ya kirafiki.

“Ninataka kuonyesha Hull City uzuri wetu. Ninajua kile timu yangu inaweza kufanya. Tuna wachezaji wazuri wenye talanta kubwa hivyo tutajituma.” Kerr alisema kwenye tovuti rasmi ya Gor.

Mechi hiyo iliandaliwa na kampuni ya pata pote ya spoti, Sportpesa mwaka mmoja baada ya timu jumuishi ya wachezaji wa soka wa humu nchini kucheza na Hull City katika uwanja wa KCOM.

No comments:

Post a Comment